Yanga Yabanwa,Yatoka sare ya 1-1 na African Lyon Ligi kuu Tanzania bara

MABINGWA watetezi Tanzania bara Yanga
wamelazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa 17 wa Ligi Kuu Soka
Tanzania bara dhidi ya African Lyon.
Katika mchezo huo uliochezwa
kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mabao yalifungwa na Ludovick
Venance wa African Lyon na Amis Tambwe kwa upande wa Yanga.
Sare
hiyo itaendelea kuibakiza Yanga kwenye nafasi ya pili ikifikisha jumla
ya pointi 37 nyuma ya vinara Simba yenye pointi 38.
Matokeo hayo
yana faida kwa Simba kama itashinda mchezo wake wa leo dhidi ya JKT Ruvu
utakaochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, itawaacha wapinzani wake kwa
tofauti ya pointi nne kwa kuwa itafikisha pointi 41.
Hata kama Simba itafungwa au kupata sare yoyote bado itaendelea kuongoza.
African Lyon ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika 59
lililofungwa na Venance baada ya kupata krosi nzuri ya Abdallah Mguhi.
Venance aliingia kipindi cha pili dakika 46 kuchukua nafasi ya Awadh Juma.
Aidha, Tambwe akaisawazishia Yanga dakika ya 74 kwa kichwa baada ya kupata krosi ya Juma Abdul.
Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kila timu haikuweza kufumumania nyavu ya mwenzake.

Yanga ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuzitumia
kupitia kwa Tambwe, Haruna Niyonzima, Vicent Bossou, Thaban Kamusoko,
Simon Msuva na Geofrey Mwashiuya huku Mguhi kwa upande wa African Lyon
akikosa pia.
African Lyon inapata sare ya pili mfululizo na
kufikisha pointi 19. Timu hii inazidi kujiwekea rekodi kwa kuzibana timu
tatu zinazoongoza ligi, ikitoka kuilazimisha Azam FC sare ya bila
kufungana na pia, iliifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya
kwanza.

Kikosi cha Yanga kilikuwa na Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul,
Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Saidi Juma, Simoni Msuva,
Thabani Kamusoko/Obrey Chirwa, Amisi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi
Kaseke/Emmanuel Martin.
African Lyon; Jehu Youthe, Miraj Adam,
Baraka Jaffary, Halfan Twenye, Hamadi Waziri, Hamadi Manzi, Hassan
Isihaka, Omary Abdallah, Awadh Juma/Ludovick Venance, Thomas Maurice na
Abdallah Mguhi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s