NISHA AFUNGUKA SABABU ZA KUDANGANYA KUWA NI MJAMZITO! NAY WA MITEGO AMTOLEA MAPOVU

Kila mmoja ilimsikitisha story ambayo mwanadada Nisha alikuwa akitupanga na kutuaminisha kuwa amebakwa na aliyekuwa mpenzi wake na kupelekea kupata ujauzito.
Kitu ambacho kilizua utata mkubwa sana na maswali ya sintofahamu na kupelekea wasanii ambao wamewahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Nisha kuingizwa katika sakata hilo akiwemo Nay wa Mitego.
Siku chache zilizopita Nisha alisikika katika vyombo vya habari akifunguka ukweli kuhusu ujauzito wake na kudai kuwa ni kazi ndiyo ilimfanya kudanganya hivyo lakini yeye sio mjamzito. Kitu ambacho kiliwatoa mapovu wengi ambao walikuwa wakimfuatilia mwanadada huyo.
Soudy Brown amepiga story na mwanadada huyo kwenye U-Heard ya leo December 22 na amefunguka mengi kuhusu kitendo chake hicho cha kudanganya umma. Soudy pia alimvutia waya Nay wa Mitego ili kutaka kujua ana kipi cha kuzungumza baada ya story hizo za mwanadada Nisha.
Ubuyu wote nimeukusanya hapa kwenye video hii hapa chini unaweza kuplay ili kuwasikiliza Nisha na Nay wa Mitego walivyo funguka.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s